LONYANGAPUO AKOSOLEWA KUTOKANA NA CHANGUO LAKE LA MGOMBEA MWENZA.

Mgombea ugavana katika kaunti hii ya Pokot magharibi Simon Kachapin amemsuta gavana wa sasa John Lonyangapuo kwa kumchagua mgombea mwenza mwenye majina sawa na yake.
Kachapin ambaye ni gavana wa kwanza wa kaunti hii amesema kuwa huenda gavana Lonyangapuo alichukua hatua hiyo kwa makusudi ili kuwakanganya wafuasi wake kumpigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Amesema kuwa atafanya mashauriano na tume ya uchaguzi IEBC ili kupata ufafanuzi zaidi kuhusiana na hatua hiyo, huku akiahidi kuwahamasisha wafuasi wake kutokanganywa na hatua hiyo ya gavana Lonyangapuo.
Wakati uo huo Kachapin ametumia fursa hiyo kujipigia debe mbele ya uchaguzi mkuu ujao akisema kuwa sasa ana tajriba ya kutosha ya kuimarisha kaunti hii baada ya kuhudumu kama naibu waziri katika serikali kuu.