Lonyangapuo ajitetea dhidi ya matumizi mabaya ya afisi

Aliyekuwa gavana wa kuanti ya Pokot Magharibi John Longangapuo, Picha/Benson Aswan
Na Benson Aswani,
Aliyekuwa gavana wa kaunti ya pokot magharibi prof. John lonyangapuo amelalamikia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matamshi ya chuki kutoka kwa wanasiasa na propaganda z inazochangia uhasama na joto la kisiasa kuongezeka nchini.
Akizungumza katika hafla moja ya mazishi eneo la Cheptuya, Lonyangapuo alisema mitandao ya kijamii inatumika vibaya kuwachafulia majina viongozi wengine nchini, hasa ikizingatiwa ni mmoja wa wale ambao wamejikuta katika hali hiyo kutokana nafasi yake akiwa gavana wa pili kaunti ya Pokot magharibi.
Gavana huyo wa zamani alitumia fursa hiyo kupuuzilia mbali madai kwamba alikamatwa kwa makosa ya matumizi mabaya ya afisa wakati akihudumu kama gavana wa kaunti hiyo, akisema kila hatua aliyochukua kuhusiana na fedha za umma ilifuata sheria.
Alisema madai dhidi yake yalilenga kumchafulia jina ili asipate fursa ya kuwania tena kiti cha ugavana wa kaunti hiyo katika uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza kwamba hatakuwa debeni tu, bali atatwaa tena kiti hicho baada ya uchaguzi.
“Niliwanunulia chakula kwa sababu njaa ilitaka kuwaua watoto wangu na kila mtu, tukafuata sheria kulingana na vile katiba inasema. Kwa hivyo msijali na lazima niulizwe ulinunuaje? Si ni lazima nijibu? Ndio niliitwa jana sasa nikaenda kusema,” alisema Lonyangapuo.
Wakati uo huo Lonyangapuo alitumia fursa hiyo kumsuta aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kwa madai ambayo amekuwa akitoa kuhusu njama ya kumwangamiza, akimtaka kudhibiti ulimi wake aliodai unaeneza uchochezi nchini.
“Kama ulishindwa kuongoza, achia wengine. Si hata sisi tulishindwa juzi? Si niko napumzika? Huyu jamaa aende apumzike. Ati Murkomen anataka kuua yeye, president aue yeye, tangu lini wakenya wanauana? Kwa hivyo huo mdomo ukome,” alisema.