LONYANGAPUO AAHIDI USHIRIKIANO WA SERIKALI YAKE NA VIONGOZI WA DINI.


Gavana wa kaunti ya Pokot magharibi John Lonyangapuo ameahidi kushirikiana kikamilifu na viongozi wa kidini katika serikali yake iwapo atachaguliwa tena kuongoza kaunti hii kwa muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti.
Akizungumza baada ya kuhudhuria ibaada ya jumapili katika kanisa la Redeemed Gospel mtaani mathare katika viunga vya mji wa makutano, Lonyangapuo alisema kuwa viongozi wa kidini ni kiungo muhimu katika kutafuta suluhu kwa changamoto zinazowakabili wananchi.
Lonyangapuo alitumia fursa hiyo kuwarai wakazi wa kaunti hii kumchagua kwa awamu ya pili kuendeleza miradi aliyoanzisha huku akipigia upatu maendeleo ambayo ameafikia katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi.
Wakati uo huo Lonyangapuo aliwataka wakazi katika kaunti hii kuwa makini na kuwapiga msasa viongozi waliotangaza nia ya kuwania viti vya kisiasa ili kuwachagua viongozi ambao watahakikisha maendeleo na kujitenga na wanaonuia kuwagawanya kwa misingi ya kikabila.