LOCHAKAPONG APONGEZA UTEUZI WAKE.


Mbunge wa Sigor katika kaunti hii ya Pokot magharibi ameahidi kushirikiana na viongozi wote eneo hilo ili kuhakikisha kuwa wakazi wa eneo hilo wananufaika kimaendeleo.
Akizungumza baada ya kuhifadhi kiti hicho, Lochakapong amewashukuru wakazi kwa kuhakikisha kuwa anahifadhi kiti hicho ili kukamilisha yale aliyoanzisha katika muhula wake wa kwanza ambao amehudumu kama mbunge wa eneo bunge hilo.
Ameahidi kuwahudumia kwa usawa wakazi wote wa eneo hilo bila kuzingatia misingi ya waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura katika uchaguzi huo.
Wakati uo huo Lochakapong amewataka wakazi wa eneo hilo kuangazia maswala ya mendeleo sasa kwani kipindi cha siasa za uchaguzi kimekamilika.