KUPPET YALALAMIKIA UPUNGUFU WA WALIMU POKOT MAGHARIBI.
Tume ya huduma za walimu TSC imetakiwa kuangazia kwa ukamilifu swala la uhaba wa walimu katika shule za kaunti hii ya Pokot magharibi wakati ambapo serikali inatekeleza sera ya kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane kcpe wanajiunga na kidato cha kwanza.
Katibu mkuu wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET tawi la kaunti hii ya Pokot magharibi Alfred Kamuto amesema kuwa shule nyingi za kaunti hii zina upungufu mkubwa wa walimu ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi hali ambayo huenda ikapelekea wanafunzi kutohudumiwa ipasavyo.
Wakati uo huo kamuto ametoa wito kwa serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanaotoa chanjo dhidi ya virusi vya corona wanazuru shule mbali mbali ili kuwarahisishia walimu shughuli ya kupokea chanjo kwani wengi wao wako sehemu ambako chanjo hizo hazijafika.