KUP CHAPUUZA MADAI YA KUTOKUWA NA UWEZO WA KUUZA AZIMIO POKOT MAGHARIBI.


Chama cha KUP katika kaunti hii ya Pokot magharibi kimepinga vikali madai kuwa hakina uwezo wa kuuza sera za chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya katika kaunti hii.
Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia anagombea useneta katika kaunti hii Geofrey Lipale amesema kuwa chama hicho kina umaarufu mkubwa katika kaunti hii ikilinganishwa na vyama vingine tanzu vya muungano huo.
Aidha amesema hali kuwa chama hicho kina wanachama wawili wa kamati ya kuongoza kampeni za Raila eneo la bonde la ufa inakipa nguvu za kuhakikisha muungano huo unapata uungwaji mkono mkubwa.
Hata hivyo Lipale amesema kuwa itakuwa kazi ngumu kutwaa ushindi katika kaunti hii iwapo kamati kuu ya muungano huo haitajitolea kuwekeza pakubwa katika kampeni hizo kirasilimali.