KUONDOLEWA KWA SHULE ZA MABWENI YAKOSOLEWA NA MBUNGE WA KAPENGURIA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamepinga vikali mipango ya serikali kuondoa shule za mabweni ilivyotangazwa na katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang.

Kipsang alisema kwamba hatua hiyo inanuia kuhakikisha kwamba wanafunzi kutoka jamii masikini pia wanapata elimu kama wenzao ikizingatiwa shule za mabweni ni ghali mno kuliko za kutwa wakati uo huo wazazi wakitekeleza majukumu yao ya malezi na kutowaachia walimu pekee jukumu hilo.

Hata hivyo pendekezo hilo limepokelewa kwa hisia tofauti nchini mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto akisema huenda hatua hiyo ikawa pigo kubwa kwa wanafunzi kutoka jamii za wafugaji ambako kunashuhudiwa utovu wa usalama pamoja na watu kuhama hama kutafuta lishe ya mifugo.

Moroto amemsuta vikali katibu Kipsang kufuatia tangazo hilo akisema kwamba wizara muhimu kama ya elimu inastahili kusimamiwa na watu ambao wanafanya uchunguzi kuhusu mazingira na matakwa ya jamii mbali mbali nchini kabla ya kufanya maamuzi.

[wp_radio_player]