KUNGOLEWA KWA NEMBO ZA CHAMA CHA UDA UNAZIDI KUSHTUMIWA NA VIONGOZI WA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBIViongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameonywa dhidi ya kutumia vijana kuzua vurugu na kuhitilafiana na mipango ya vyama vingine kwa malengo yao ya binafsi.
Aliyekuwa gavana wa kaunti hii Simon Kachapin amesema kuwa viongozi wanafaa kuvumiliana hasa wakati huu taifa linapoeleka katika uchaguzi mkuu ujao, huku akionya kuwa huenda hali ikawa mbaya zaidi iwapo visa kama hivi havitadhibitiwa mapema.
Kachapin ametaja visa hivyo kuwa kitendo cha uwoga, kwani baadhi ya viongozi ambao wapo mamlakani kwa sasa wameanza kuonyesha hofu ya kushindwa na wapinzani wao katika uchaguzi wa mwezi agosti na sasa wanadhihirisha woga wao kupitia kuzua vurugu.
Amewataka vijana katika kaunti hii kutokubali kutumika visivyo na wanasiasa na badala yake kudumisha amani kwa kumpa kila kiongozi nafasi ya kuuza sera zake licha ya tofauti za vyama kwani kila chama kina uhuru wa kuuza sera zake kwa kutumia mbinu yoyote ile.

[wp_radio_player]