KUKAMATWA MAJAJI WAWILI KWAZIDI KUKASHIFIWA.
Hisia mseto zimeendelea kuibuliwa miongoni mwa wananchi kufuatia hatua ya maafisa wa DCI kuwatia mbaroni majaji wawili Aggrey Mchelule na Said Chitembwe juma jana na kuwahoji kabla ya kuwaachilia muda mfupi baadaye.
Baadhi ya wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wamedai kuwa huenda huu ni mpango wa serikali kutafuta njia ya kujitakasa kwa kuwafanya wananchi waamini madai yaliyoibuliwa na rais Uhuru Kenyatta kuhusu baadhi ya majaji aliodinda kuwapandisha vyeo.
Aidha baadhi ya wakazi wamehusisha kukamatwa kwa majaji hao na hatua ya majaji watano wa mahakama kuu kuharamisha mchakato mzima wa kufanyia katiba marekebisho kupitia mpango wa upatanishi BBI.