KUBANDULIWA MUKENYA KAMA SPIKA KWAENDELEA KUCHOCHEA HISIA.


mseto zimeendelea kuibuliwa katika kaunti hii ya pokot magharibi kufuatia hatua ya bunge la kaunti hii kumbandua afisini spika Catherine Mukenyang kwa madai ya utumizi mbaya wa afisi miongoni mwa tuhuma zingine zilizoibuliwa dhidi yake.
Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni mgombea kiti cha ubunge eneo bunge la Kacheliba katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao John Lodinyo ambaye ameshutumu hatua hiyo ya wabunge katika bunge hilo hasa ikizingatiwa Mukenyang alikuwa amesalia na muda mchache kabla ya kujiuzulu.
Lodinyo amepuuzilia mbali madai yaliyobuliwa na waakilishi wadi dhidi ya mukenyang akiyataja kuwa yasiyo na msingi wowote huku akidai kuwa msukumo wa kumwondoa Mukenyang afisini ulichochewa pakubwa kisiasa.
Lodinyo ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii kutopotoshwa kisiasa na baadhi ya wanasiasa wenye malengo ya binafsi huku akimhimiza Mukenyang kutotikisika na uamuzi huo wa bunge la kaunti katika afari yake ya kuwania kiti cha mwakilishi kina mama kaunti hii.