KUBADILISHWA ULINZI WA NAIBU RAIS KWAZIDI KUIBUA HISIA NCHINI.


Mjadala kuhusu kubadilishwa vitengo vya ulinzi wa naibu rais William Ruto umeendelea kushuhudiwa nchini wandani wa Ruto wakiendelea kukashifu hatua hiyo wanayotaja kuwa inayolenga kuhujumu utendakazi wa afisi ya naibu rais.
Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti hii ya pokot magharibi Simon Kalekem ambaye amesema afisi ya naibu rais ni taasisi ya kikatiba na inayopasa kuheshimiwa na viongozi wote nchini.
Kalekem ametoa wito kwa viongozi nchini kuendesha ushindani wa kisiasa kwa njia ya kidemokrasia na kujitenga kutumia mbinu ambazo huenda zikahujumu utendakazi wa afisi ya naibu rais William Ruto kutokana na tofauti za kisiasa.