KPLC YAONYA DHIDI YA ‘WIZI’ WA NGUVU ZA UMEME POKOT MAGHARIBI

Kampuni ya Kenya Power kaunti hii ya Pokot magharibi imeonya vikali wakazi dhidi ya kuunganisha umeme kinyume cha sheria ikisema watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za sheria.
Meneja wa biashara wa kampuni hiyo kaunti hii Milimo Musavi amesema kuwa mbali na kuisababishia hasara kampuni hiyo, hatua hiyo inahatarisha maisha ya wanaofanya hivyo pamoja na wanaokaa karibu nao.
Aidha amekana madai kuwa ni maafisa kutoka kampuni ya KPLC ndio wanaotumika kuunganisha umeme kinyume cha sheria akisema wengi wanaofanya uovu huu ni vijana ambao wanapokea masomo kutoka taasisi mbali mbali na hatimaye kukosa ajira.