KOOME AENDELEA KUSHINIKIZWA KUONDOKA KATIKA KAMATI ANDALIZI YA UCHAGUZI.
Siku moja tu baada ya jaji mkuu Martha Koome kushikilia msimamo kwamba hatajiondoa kutoka kamati andalizi ya uchaguzi mkuu ujao zaidi ya wawaniaji mia mbili wa nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye chama cha UDA katika kaunti ya Trans nzoia wamemrai Koome kuwazia upya msimamo wake.
Viongozi hao akiwamo Julias Tunduria Philemon Samoei na John Njuguna wamekariri kwamba kuwapo kwake katika kamati kumesababisha mgongano wa kimajukumu.
Ikumbukwe jaji Koome alipuuza wito huo akisema kamati hiyo haina wanasiasa ambao wanaweza kuhujumu uhuru wa idara ya mahakama katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.