KONTENA ZA BIASHARA MAKUTANO ZAELEKEA KUKAMILIKA.
Matayarisho ya kontena za kufanyia biashara mjini makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi yanaelekea kukamilika .
Haya ni kwa mujibu wa afisa katika wizara ya biashara kaunti hii Lucy Lipale ambaye aidha amesema kuwa zaidi wafanyibiashara 600 wametuma maombi ya kutaka kutengewa nafasi licha ya kuwa ni kontena 70 pekee zilizopo akielezea haja ya kuweka zingine.
Lipale amesema kuwa watalazimika kufanya mchujo wa majina ya waliotuma maombi kabla ya kutoa nafasi kwa wafanyibiashara ambao watakuwa wamechaguliwa kwa kuzingatia usawa katika zoezi zima.
Wakati uo huo lipale amesema kuwa sacco za magari ya usafiri wa umma ya masafa marefu yatatengewa sehemu mbadala ya kuegesha magari yao ili kuyaondoa katikati ya mji wa makutano.