KIWANDA CHA KUSINDIKA ASALI CHAZINDULIWA LOMUT.
Shirika la NRT kwa ushirikiano na mashirika mengine limezindua kitengo cha kusindika asali honey Processing unit eneo la Lomut katika kaunti hii ya Pokot Magharibi katika juhudi za kuhakikisha kuwa wakulima wa asali wanawezeshwa zaidi.
Akizungumza wakati wa kuzindua kitengo hicho kupitia mradi wa ustahimilivu ambao umekuwa ukiendelezwa na mashirika hayo, mkurugenzi wa NRT kaunti hii Kadir Boru amewataka wakulima wa asali kutumia kitengo hicho ili kuimarisha kilimo chao.
Waziri wa kilimo na mifugo kaunti hii Evans Menach ameusifia mradi huo ambao amesema kwamba umewanufaisha pakubwa kiuchumi wakazi hasa kutoka maeneo kame, akiahidi kuwa serikali ya kaunti hii itaendelea kushirikiana na wafadhili kufanikisha miradi muhimu kama huu.
Wafugaji wa nyuki eneo hilo wakiongozwa na Christopher Makilap wameelezea kunufaika zaidi na mradi huo kwani kupitia ufadhili wa mashirika hayo wameweza kupata soko la bidhaa zao mbali na kuimarika uchumi.