KIWANDA CHA KUCHINJA NGOMBE CHA NASUKUTA CHA ZINDULIWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Uzinduzi wa kichinjio cha Nasukuta katika kaunti hii ya Pokot magharibi ni moja ya ajenda kuu za serikali ya jubilee ikiwa ni pamoja na utoshelezaji wa chakula hasa katika sekta ya kilimo biashara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa aidha amesema kuwa kichinjio hicho kitapelekea ajira kwa wakazi wengi hivyo kuwawezesha kuwa na pato la kila siku hali itakayopelekea kuimarika uchumi wa kaunti hii.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye aidha ameahidi kuanzishwa kwa mafunzo ya jinsi ya kuendesha shughuli katika kiwanda hicho huku akitoa wito kwa washirika wa serikali yake kwenye mradi huo kuleta maji katika kiwanda hicho.
Kwa upande wake afisa katika shirika la EU Emyra Bernady ambaye ni mshirika mkuu katika mradi huo amesema mradi huo utapelekea kuimarika zaidi soko la mifugo huku akiahidi kuhakikisha kuwa maji yanapatikana kwa urahisi hasa ikizingatiwa changamoto ya maji kaunti hii.