KITUO CHA UPASUAJI CHAZINDULIWA KAPENGURIA.


Kituo cha kufanya upasuaji wa magonjwa sugu kimezinduliwa rasmi hii leo katika hospitali ya kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi uzinduzi ambao umeongozwa na gavana John Lonyangapuo.
Lonyangapuo amesema kuwa kuzinduliwa rasmi kituo hicho sasa kutawapunguzia gharama ya kusafiri nje ya kaunti hii wagonjwa ambao wanatafuta huduma za upasuaji akiongeza kuwa chumba cha wagonjwa mahututi pia kinakaribia kukamilika.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na daktari mkuu katika hospitali hiyo David Karuri ambaye pia amesema hospitali hiyo imekuwa ikipokea takriban wagonjwa 10 wanaohitaji upasuaji kila mwezi akielezea matumani kuwa hospitali hiyo itafikia viwango vya kutambulika nchini katika upasuaji.