KISIERO APONGEZA MATOKEO YA KCSE ENEO LA ENDEBES TRANS NZOIA


Mwakilishi wadi wa Endebess ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Trans-nzoia ameelezea kuridhishwa kwake kutokana na matokeo bora ambayo yamesajiliwa katika shule mbalimbali katika mtihani wa kitaifa wa kcse mwaka wa 2020 kwenye wadi ya endebess na kaunti hiyo nzima.
Kwenye mkao na wanahabari mjini endebess Kisiero amesema licha ya changamoto za janga la covid 19 matokeo ya mwaka huu ni bora ikilinganishwa na miaka ya awali kwani wanafunzi wengi haswa kutoka shule za eneo bunge la endebess wameweza kujipatia nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu vya umma nchini.
Aidha Kisiero ametoa wito kwa mwanafunzi watakaokosa nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu nchini, kujisajili katika vyuo vya kiufundi pamoja na vile vya anuwai ili kujipatia ujuzi wa kiufundi jambo analosema litasaidia katika kutoa nafasi za ajira kwa vijana wengi badala ya kutegemea kuajiriwa.