KISA CHA WABUNGE SIMBA ARATI NA SILVANUS OSORO KURUSHIANA MAKONDE CHA ENDELEA KUSHTUMIWA VIKALI


Wafuasi wa naibu wa rais Wiliam Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga walioko kwenye kaunti ya Pokot Magharibi wamekishutumu vikali kisa cha kukabiliana kwa makonde kwa mbunge wa Dagorreti Kusini Simba Arati na mwenzake wa Mugirango Kusini Silvanus Osoro kwenye mazishi ya babake Naibu gavana wa Kisii Joash Maangi.
Wafuasi hao wamemkosoa Simba Arati kwa kurejelea machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka elfu mbili na saba wakitaja kwamba kutachochea uhasama baina ya wakenya kwa ujumla.
Wamesema sio utu kushiriki kwenye mapigano hasa wakiwa kwenye maombolezi.
Wamemtaka Rais Kenyatta na idara nyingine za uchunguzi kuwachukulia hatua za kisheria wawili hao ili iwe funzo kwa wanasiasa wengine nchini.