KIPTIS APONGEZWA KWA KUFANYIA MAGEUZI WIZARA MBALI MBALI KAUNTI YA BARINGO.


Gavana kaunti ya Baringo Stanley Kiptis anaendelea kupongezwa kutokana na mageuzi aliyofanya katika wizara mbali mbali ambapo maafisa wakuu wa wizara hizo walipewa uhamisho.
Kwenye kikao na wanahabari mjini Kabarnet mwakilishi wadi ya mochongoi Kipruto Kimosop amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kuimarika huduma katika wizara tofauti na hasaa ile ya barabara.
Kimosop amesema kuwa afisa mkuu aliyekuwa akihudumu kwenye wizara hiyo michael kiptoo alifeli kutekeleza majukumu yake ipasavyo hivyo kuchangia kukwama kwa miradi muhimu ya ukarabati wa barabara.
Kimosop aidha amemtaka afisa mkuu wa sasa kwenye wizara hiyo Moses Lokidor kuhakikisha kwamba miradi yote ya barabara iliyosimama inarejelewa na kukamilishwa kwa wakati.