KIONGOZI WA WENGI KATIKA BUNGE LA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AFARIKI DUNIA AKIPOKEA MATIBABU MJINI ELDORET
Huzuni imetanda miongoni mwa wakazi wa Kaunti ya Pokot Magharibi hasa wakazi wa Wadi ya Sekerr kufuatia kifo cha ghafla Cha Mwakilishiwadi wao ambaye pia amekuwa ndiye Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi, Thomas Ng’olesia Amutang’orok.
Seneta wa Kaunti hii Dkt. Samuel Poghisio amekuwa kiongozi wa kwanza kumwomboleza huku akimtaja kuwa kiongozi shupavu ambaye amekuwa akipigania ufisadi na masuala mengine muhimu Katika bunge hilo.
Kulingana na Poghisio, marahemu aliugua kwa ghafla akilalamikia maumivu ya tumbo kabla ya kukimbizwa kwenye Hospitali ya St. Lukes kule Eldoret ambapo baadaye alifariki dunia mikononi mwa madaktari.
Poghisio amesema familia na marafiki wote wa Chama Cha KANU wamempoteza tegemeo kubwa wa chama hicho.
Naibu Gavana wa Pokot Magharibi Dkt. Nicolas Atudonyang’ vilevile ametuma rambirambi zake kwa njia ya Mtandao wa Facebook akimsifia mwenda zake kwa jitihada ambazo amekuwa akizifanya katika kujipigia na kukiimarisha Chama Cha KANU katika Kaunti ya Pokot Magharibi.
Mwili wake unahifadhiwa katika chumba kimoja Cha maiti mjini Eldoret huku mipango yote ya mazishi yakitarajiwa kufanywa na kamati ya Bunge la Kaunti ya Pokot Magharibi.