KINARA WA CHAMA CHA ODM RAILA ODINGA ATHIBITISHWA KUAMBUKIZWA VIRUSI VYA CORONA


Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amedhibitishwa kuambukizwa virusi vya corona siku 3 tu baada ya kulazwa katika hospitali ya Nairobi.
Kulingana na daktari wake Odinga, David Oluoch Olunya ni kwamba kwa sasa anaendelea kupokea matibabu huku hali yake ikiimarika.
Viongozi mbali mbali akiwemo naibu wa rais William Ruto, seneta wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, seneta maalum Millicent Omanga wamemtakia afueni ya haraka.
Kupitia mtandao wake wa twitter Odinga amesema kuwa atafuata ushauri wa daktari wake na kujiweka kwenye karantini kwa kipindi kinachohitajika.
Hata hivyo amewashauri wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya wizara ya afya ii kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.