KINA MAMA WATAKA KUPEWA FURSA YA KUONGOZA KATIKA NYADHIFA ZA SIASA.

Na Benson Aswani
Ni wakati kina mama pia wanastahili kupewa fursa ya uongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kwa mujibu wa mgombea kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kapenguria kaunti hii Philo Chelang’at ambaye amesema kuwa eneo bunge hili limetawaliwa kwa kipindi kirefu na wenzao wa kiume na sasa wakazi wa eneo bunge hili wanastahili kujaribu uongozi wa mwanamke.
Wakati uo huo Chelang’at ametoa wito kwa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi hasa maeneo ya mipakani ambako kumekuwa kukishuhudiwa utovu wa usalama kudumisha amani na kutoruhusu kutumika na wanasiasa kuendeleza visa vya uhalifu.