KILIO CHA WAKAZI WA KACHELIBA KUHUSU BARABARA CHAJIBIWA

Siku chache tu baada ya wakazi wa Kacheliba kaunti ya Pokot magharibi kulalamikia hali mbovu ya barabara ya kutoka Kacheliba hadi Nakuyen, mwakilishi wadi wa eneo hilo Robert Komole ametoa wito kwa wakazi hao kuwa watulivu wakati wakiendelea kuweka mikakati ya kuikarabati barabara hiyo.

Komole amesema kuwa kwa sasa kiasi fukani cha fedha kimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo japo akikiri huenda ikawa changamoto kuikarabati barabara hiyo kutokana na mvua kubwa ambayo inaendelea kushuhudiwa eneo hilo.

Aidha Komole amesema kuwa tayari mwanakandarasi atakayekarabati barabara hiyo ametambuliwa na wakati wowote atakuwa anaanza majukumu yake.