KIKAO CHA WAZEE KAUNTI YA UASIN GISHU ILI KULETA AMANI

UASIN GISHU

Wazee wa jamii mbalimbali kwenye kaunti ya Uasin Gishu wanapanga kuandaa mkutano wa pamoja ili kujadili hatua watakazopiga ili kuhakikisha amani inadumu katika kaunti hiyo.
Wakizungumza mjini Eldoret wazee hao wamewataka wakaazi wa kaunti hiyo wazungumze kwa pamoja hatua wanayosema itasaidia jamii mbali mbali kuishi kwa amani katika kaunti hiyo.

Wakiongozwa na Joseph Wainaina na John Mursi, wamesema wamechukua nafasi yao kama wazee katika jamii na kamwe hawatakubali kumwuunga mwanasiasa yeyote mchochezi haswa wakati wa kutafuta wadhifa wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka alfu mbili na ishirini na mbili.