KHAEMBA ATOA CHANGAMOTO KWA MRIDHI WAKE KUMPIKU KIMAENDELEO.
Gavana wa kaunti ya Trans nzoia Patrick Khaemba ambaye anakamilisha hatamu yake ya uongozi amemrai gavana wa pili atakayechaguliwa kuongoza kaunti hiyo kujibidiisha kutekeleza miradi zaidi ya alivyofanya katika mihula yake miwili ya ugavana katika kaunti hiyo.
Akihutubu wakati wa ufunguzi wa kituo cha kisasa cha kuegesha magari mjini Kitale, gavana Khaemba alisema kuwa anaondoka mamlakani akionea fahari ujezi wa soko la kisasa la wafanyibiashara zaidi ya 3000 na hospitali ya rufaa ambayo sehemu moja itaanza kutoa huduma za matibabu.
Aidha Khaemba alimpa changamoto gavana atakayemridhi kuendelea kudumisha umoja miongoni mwa wakazi wa kaunti hiyo yenye makabila mengi, kupiga jeki sekta ya kilimo na kupunguza kiwango cha umasikini kwa kuboresha maisha ya wakazi.