KHAEMBA ALAUMIWA KWA UTENDAKAZI DUNI TRANS NZOIA.


Viongozi kutoka kaunti ya Trans-nzoia wamelalamikia utenda kazi duni wa serikali ya kaunti hiyo kwa kile wamesema imekosa kuwajibikia wenyeji.
Wakiongozwa na mbunge wa endebess Dkt Robert Pukose viongozi hao wametaka serikali ya kaunti hiyo kupitia wizara ya afya kusuluhisha kwa haraka tatizo la maji katika hospitali ndogo ya Endebes ambayo imekosa maji kwa zaidi ya majuma mawili sasa.
Pukose amependekeza kubuniwa kwa mfuko maalum wa fedha katika wizara ya afya utakaowezesha hospitali mbalimbali kujisimamia kwa shughuli za dharura hospitalini badala ya kutegemea fedha kutoka kwa serikali ya kaunti pekee.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa akimtaka gavana Patrick Khaemba kujukumika na kukamilisha miradi yote aliyoanzisha hii ikiwa ni pamoja na hospitali ya rufaa, uwanja wa michezo wa Kenyatta na soko kuu mjini Kitale.
Aidha amemtaka Khaemba kufika mbele ya kamati ya bunge la kaunti hiyo kuhusu uhasibu na kuelezea umma kuhusu matumizi ya mabilioni ya fedha ambazo zimefika kaunti hiyo.