KHAEMBA ALAUMIWA KWA KUTOFANIKISHA MAENDELEO TRANS NZOIA.


Spika wa bunge la kaunti ya Trans nzoia Joshua Werunga amemlaumu gavana wa kaunti hiyo Patrick Khaemba kwa kutofanikisha miradi ya maendeleo licha ya serikali ya kaunti hiyo kutengewa mgao wa zaidi ya shilingi bilioni 60 tangu kuanzishwa kwa ugatuzi.
Werunga amesema kuwa wanaotilia shaka utendakazi wake wa bunge na kulinganisha na azma yake ya kuwania wadhifa wa useneta hawaelewi majukumu ya bunge la kaunti na serikali tendaji yani the executive.
Hata hivyo Khaemba amesema kuwa juhudi zake za kukamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa, kituo cha kisasa cha kuegesha magari, soko la kisasa na kuwapa hati miliki wakazi imekuwa ikikwamishwa na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao ya binafsi.
Kuhusu utoshelezi wa chakula Werunga amesema serikali inapasa kuwapa maskwata vipande vya ardhi ili kuzalisha chakula.