KFS YAWAHAMISHA MAAFISA WAKE WOTE BAADA YA MAUAJI YA WATU WAWILI ELGEYO MARAKWET.


Shirika la huduma za misitu KFS limewahamisha maafisa wote katika kituo cha kulinda misitu cha Elgeyo forest katika kaunti ya Elgeyo Marakwet kufuatia mauaji ya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa.
Kamanda wa shirika hilo Kennedy Kalinya amesema maafisa wapya wanatarajiwa katika kituo hicho wakati wowote akiongeza kuwa tayari idara ya upepelezi DCI imeanzisha uchunguzi kufuatia mauaji hayo.
Viongozi wa kaunti hiyo wakiongozwa na gavana Alex Tolgos wameendela kushutumu mauaji hayo wakisema maafisa wa KFS walikosea kwa kuwafyatuliwa risasi wenyeji.
Naibu gavana wa kaunti hiyo Wesley Rotich amesema kuwa kwa miaka mingi maafisa wa KFS katika kituo hicho wamekuwa wakiwanyanyasa raia bila hatua zozote kuchukuliwa akishinikiza uchunguzi kuharakishwa ili familia zilizoathirika wapate haki.