KFS YASHUTUMIWA KWA UKANDAMIZAJI SABOTI, TRANS NOZIA


Wakazi wa eneo bunge la saboti kaunti ya Trans nzoia wamelalamikia kukandamizwa na uongozi wa shirika la uhifadhi misitu KFS.
Wakiongozwa na Luke Naibei wakazi hao wamesema baadhi ya maafisa wa shirika hilo wanatumia njia za mkato kuwateua viongozi wa chama cha kijamii cha kuhifadhi msitu huo na kuwatoza ada wakazi hao bila kuwapokeza risiti kwa ahadi kuwa watajumuishwa katika mpango wa shamba system.
Aidha Luke ameelezea kughadhabishwa na hatua ya maafisa hao kuwatia nguvuni wakazi mara kwa mara wakilenga kuwakandamiza katika kutetea haki zao.