KENYA SEED YAHAKIKISHIA WATEJA WAKE MBEGU ZA KUTOSHA MSIMU WA UPANZI.


Huku msimu wa upanzi ukitazamiwa kuanza maeneo mbalimbali humu nchini Kampuni ya uzalishaji mbegu nchini Kenya Seed imewahakikishia wakulima kuwa kuna mbegu za kutosha kwa mahitaji ya wakulima humu nchini na kwenye masoko ya mataifa jirani kwa upanzi mwaka huu.
Kwenye kikao na wanahabari baada ya mkutano na wasambazaji na wauzaji wa mbegu mjini Kitale Meneja msimamizi wa kampuni hiyo Fred Oloibei amesema kuwa anamatumaini kuwa msimu huu utakuwa bora zaidi kwa wakulima ikilinganishwa na miaka iliyopita kutokana na dalili za mvua ya mapema msimu huu.
Wakati huo huo Oleibei amesema Kampuni hiyo imeweka mikakati ya kutosha kukabiliana na tatizo la mbegu ghushi kama njia moja ya kuzuiya hasara kwa wakulima nchini.