KENYA POWER YALAUMIWA KWA UTEPETEVU KACHELIBA.

Na Benson Aswani
Wakazi wa eneo la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kulalamikia ukosefu wa nguvu za umeme eneo hilo kwa muda sasa.
Wakiongozwa na Joseph Sarich wakazi hao wamesema kuwa shughuli zao nyingi za kila siku zinazotegemea umeme zimeathirika pakubwa na licha yao kulalamikia kampuni ya Kenya power mara kwa mara hamna hatua yoyote ambayo imechukuliwa kufikia sasa.
Wakazi hao sasa wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kuingilia kati na kusuluhisha hali hiyo huku wakipendekeza maafisa wa kampuni hiyo katika kaunti hii ya Pokot magharibi kubadilishwa na kuajiriwa maafisa ambao watazingatia majukumu yao kikamilifu.