‘KENYA KWANZA ITAKABILI UTOVU WA USALAMA BONDE LA KERIO’, WASEMA VIONGOZI WA UDA.

Viongozi wanaowania nyadhifa za uongozi katika kaunti ya baringo kupitia chama cha UDA, wameelezea matumaini kwamba serikali ya kenya kwanza itashughulikia tatizo la utovu wa usalama unaochangiwa na visa vya wizi wa mifugo.
Wakiongea kwenye hafla ya maombi ya shukrani mjini kabarnet viongozi hao wakiongozwa na gavana wa kwanza kaunti hii Benjamin Cheboi wamesema kuwa naibu rais Dkt william Ruto ameahidi kushughulikia tatizo hilo iwapo ataibuka mshindi kwenye uchaguzi wa agosti 9.
Hata hivyo viongozi hao wamekariri kwamba pana haja ya kuwapo ushirikiano baina yao ili kujadili mbinu zinazoweza kusaidia kurejesha utulivu kwenye baadhi ya maneo ya Baringo kusini na kaskazini.
Naye mwaniaji ubunge eneo la Tiaty Peter Ngeleyo amesema kuwa jamii nzima haifai kuangaziwa kama inayotekeleza wizi wa mifugo kwani ni watu wachache tu wanaojihusisha na uhalifu huo.
Aidha kwa upande wake seneta kaunti ya Elgeyo marakwet Kipchumba Murkomen amesema kuwa utovu wa usalama katika eneo la bonde la Kerio utakabiliwa iwapo miradi tofauti ya maendeleo itatekelezwa eneo maeneo hayo.