KENGEN YASHUTUMIWA KWA KUWAHANGAISHA WAKAZI TURKWEL.


Kampuni ya kuzalisha umeme ya KENGEN imeshutumiwa vikali kwa jinsi inavyoendesha shughuli zake eneo la Turkwel katika kaunti hii ya Pokot magharibi huku ikidaiwa kuwahangaisha wakazi wa eneo hilo.
Wakizungumza katika hafla moja eneo hilo viongozi wa kaunti hii wakiongozwa na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto wameelezea ghadhabu zao kwa kile wamedai wakazi wanaoishi karibu na kampuni hiyo wameagizwa kuondoka huku wakimtaka waziri wa kawi Charles Keter kuingilia kati.
Wakati uo huo viongozi hao wamekosoa ukarabati wa baadhi ya shule ambao umeendeshwa na kampuni ya KENGEN, wakidai kuwa kampuni hiyo imefanya kazi duni huku wakitishia kuongoza maandamano kulalamikia kile wamedai kampuni hiyo inahujumu elimu.
Kwa upande wake spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang ametoa wito kwa viongozI hasa a kike na wahisani zaidi kujitokeza ii kusaidia katika kusambaza visodo kwa wanafunzi wa kike eneo hilo hasa wakati huu ambapo shule zimefunguliwa kwa muhula wa kwanza.