KAUNTI ZA BONDE LA KERIO ZATAKIWA KUKUMBATIA AMANI.


Gavana wa Baringo Starnely Kiptis amewashauri wakaazi wa maeneo ya bonde la kerio na kaunti nyingine ambazo zinashuhudiwa wizi wa mifugo kusitisha uhasama na kuishi kwa amani.
Kiptis amesema kwamba mashambulizi mengi yanachochewa na umiliki wa ardhi ya malisho ya mifugo.
Aidha amedokeza kwamba ukosefu wa elimu na ajira miongoni mwa wakaazi vilevile umechangia kutokuwa na makubaliano baina ya jamii zinazoishi kwenye eneo hilo akisema kujengwa kwa shule kwenye maeneo hayo kutasaidia pakubwa kukabili hali hiyo.
Kiptis amesema viongozi wa maeneo yaliyoathirika wamekuwa wakijaribu kila mbinu kuhakikisha kuwa amani inarejeshwa miongoni mwa mikakati hiyo ikiwa kuendeleza kwa miradi ya maendeleo kwenye maeneo hayo, kuboreshwa kwa mifugo na hata kuendelezwa kwa kilimo cha mimea mbalimbali ili kuhakikisha kwamba mapato ya wakazi yanaimarishwa.