KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAPOKEZWA DAWA ZA KIMA CHA SHILINGI M 44.6.
Ni afueni kwa wakazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi baada ya serikali ya kaunti hii kupokea dawa za kima cha shilingi milioni 44.6 kutoka kwa mamlaka ya kusambaza dawa na vifaa vya matibabu kemsa.
Akizungumza katika hafla ya kupokeza serikali ya kaunti dawa hizo msimamizi wa mamlaka hiyo kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa Zacheus Muya amesema kaunti hii itapewa kipau mbele katika usambazaji wa dawa hizo siku za usoni kwani ina mahitaji ya kipee ikilinganishwa na kaunti zingine nchini.
Akipokea dawa hizo gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo amesema serikali yake itahakikisha kila kituo cha afya na zahanati inasambaziwa dawa kulingana na maombi iliyotuma huku akionya vikali dhidi ya matumizi mabaya ya dawa hizo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na waziri wa afya kaunti hii Christine Apakoreng ambaye aidha amezitaka kamati za zahanati hizo kuwa makini na jinsi dawa hizo zinatumika ili kuhakikisha kuna uwazi katika matumizi yake.