KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUSHUHUDIA MVUA CHACHE MWAKA HUU KUTOKANA NA MABADILIKO YA HALI YA ANGA


Ni wazi kuwa mwaka huu hakutashuhudiwa kiwango cha kutosha cha mvua ikilinganishwa na mwaka jana.
Haya ni kulingana na katibu katika wizara ya ugatuzi na maeneo kame Mika Powon ambaye alikuwa akizungumza eneo la Chepkobe kaunti hii ya Pokot magharibi ambapo amesema kuwa hali hii imetokana na mabadiliko ya hali ya anga.
Powon amewahimiza wakulima katika kaunti hii kuhifadhi chakula cha matumizi pamoja na chakula cha mifugo ili kuhakikisha hawapitii mahangaiko kufuatia ukame kwani huenda kusishuhudiwe mvua ya kutosha hivi karibuni hadi mwezi Septemba.
Wakati uo huo amesema kuwa serikali kuu inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa watakaoathirika hasa kwa kukosa chakula wanasaidiwa, huku pia akitoa wito kwa serikali za kaunti kuhakikisha kuwa zinatenga fedha katika bajeti yake zitakazotumika kuwasaidia waathiriwa.