KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI KUJADILI MSWADA WA MAREKEBISHO YA KATIBA WA 2020 NA KUUPIGIA KURA HII LEO


Huku mabunge ya kaunti mbalimbali nchini yakizidi kujadili mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka wa 2020 kupitia ripoti ya BBI, wawakilishi wadi kwenye bunge la kaunti ya pokot magharibi wanatarajiwa kujadili na kupigia kura mswada huo hii leo.
Kwa mujibu wa mwakilishi wadi ya Riwo David Alukulem ni kuwa wawakilishi wadi wote wako tayari kutoa maoni yao kuhusiana na mswada huo kabla ya kupiga kura itakayo amua hatima ya BBI.
Kiongozi huyo hata hivyo amewataka wakenya kupuuza propaganda kuwa raisu huru Kenyatta aliwapa hongo kupitia ufadhili wa shilingi milioni 2 ya kununua gari yaani car grant iliwapitishe BBI.
Ikumbukwe kuwa gavana wa kaunti hii Profesa John Lonyangapuo pamoja na wabunge na viongozi wengine wamekua mstari wambele kuwashawishi wakaazi wa eneo hili kuunga mkono BBI wakisema italeta manufaa makubwa kwenye jimbo hili ikiwemo kuongezwa kwa eneo bunge moja zaidi.
Hata hivyo mbunge wa Kapenguria Samwel Chumel Moroto alionekana kuupinga mswada wenyewe.