KAUNTI KAME NCHINI ZATARAJIWA KUNUFAIKA NA MIRADI ZAIDI KUTOKA SERIKALI YA USWIZI.

Serikali ya uswizi itaendelea kushirikiana na serikali za kaunti kame nchini kupitia miradi mbali mbali ili kukabili hali ngumu ambayo wakazi hukumbana nayo kutokana na hali ya ukame ambao unashuhudiwa kwenye kaunti hizi.

Akizungumza baada ya kukagua miradi mbali mbali inayoendelezwa na serikali hiyo kaunti  ya Pokot magharibi kupitia shirika la World Vision, balozi wa uswizi nchini Caroline Bishini alisema miradi hiyo inakusudiwa kukabili athari za hali ya anga kwa wakazi wa kaunti hizo.

“Serikali ya uswizi itaendelea kushirikiana na kaunti kame nchini kupitia miradi mbali mbali ili kuhakikisha kwamba hawakumbwi na athari za mabadiliko ya hali ya anga.” Alisema Bishini.

Bishini alisema kwamba miradi hiyo ambayo inaendelezwa kupitia mpango wa imara inalenga kuhakikisha kwamba wakazi wa kaunti hii wanawezeshwa kiuchumi ili kuimarisha maisha yao pamoja na ya watoto wao.

“Nina imani kwamba miradi hii ambayo inaendelezwa kupitia mpango wa imara itasaidia kuhakikisha kwamba wakazi wa kaunti hii wanaimarika kiuchumi.” Alisema.

Gavana wa kaunti ya Pokot magharibi Simon Kachapin aliipongeza serikali ya taifa hilo la uswizi kwa kile alitaja kuwa uwekezaji mkubwa katika miradi mbali mbali kaunti hiyo ambayo inalenga kuimarisha zaidi maisha ya wananchi.

“Serikali ya uswizi imewekezwa pakubwa katika kaunti hii kupitia miradi mbali mbali ambayo inalenga kuimarisha maisha ya wananchi. Nafurahia sana ushirikiano huu ambao ni wa manufaa makubwa kwa watu wetu.” Alisema Kachapin.