KASISI AMSHAMBULIA MWANAFUZNI KUHUSU MZOZO WA ARDHI TRANS NZOIA

Na Benson Aswani
Wazazi na walimu kutoka shule ya msingi kese wadi ya keiyo eneo bunge la kwanza katika kaunti ya Trans nzoia wamelaani vikali kisa ambapo kasisi wa kanisa moja eneo hilo alimshambulia mwanafunzi kwa kumkata kwa upanga alipokuwa na wenzake wakifyeka uwanja wa shule yao.
Kulingana na mwanafunzi aliyeshambuliwa na kasisi huyo akiongea na wanahabari akiwa kwenye zahanati ya kapkoi kasisi wa kanisa la reformed church of east Africa peter masai alimshambulia wakati walipokuwa wakifyeka uwanja wa shule yao pamoja na wenzake kwa maandalizi ya michezo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Thomas makoha ameelezea kuwepo na mzozo wa shamba la shule na usimamizi wa kanisa hilo ambapo shamba la shule lilinyakuliwa na kasisi huyo akiomba serkali kuingilia kati kutatua mzozo huo.
Ni kisa ambacho kimeshutumiwa na wazazi eneo hilo wakisema ni cha aibu kwa mtu wa hadhi kama ya kasisi.
Hata hivyo juhudi za kumpata kasisi huyo ziliambulia patupu kwani alidinda kuzungumza na wanahabari.