KANISA LASHAURIWA KUOMBEA VIONGOZI NA TAIFA HUKU UCHAGUZI MKUU UKIKARIBIA


Mshauri mkuu wa kisheria katika afisi ya Naibu wa Rais Dkt Abraham Singoei ametoa wito kwa kanisa kuendelea kuombea viongozi na taifa hili.
Wito wake unajiri kufuatia matukio yalioshuhudiwa kwenye chaguzi ndogo zilizokamilika Siku chache zilizopita ambapo fujo na vurugu zilishuhudiwa.
Akihutubu katika kanisa la AIC Gutongoria wadi ya Sirende eneo bunge la Kiminini, Dkt Singoei amesema vurugu zilizoshuhudiwa kwenye chaguzi hizo hazikuonyesha picha nzuri ikizingatiwa taifa linakaribia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.