KANISA LA FULL GOSPEL LAJITENGA NA MAMA ALIYEJIFANYIA HARUSI CHELANG’A.
Siku chache tu baada ya mama mmoja kutoka eneo la Kalorema kujifanyia harusi mwenyewe katika bustani ya Chelang’a mjini Makutano kwa madai aliagizwa kufanya hivyo na mwenyezi Mungu, kanisa la full gospel alilohusishwa nalo mama huyo limejitenga naye.
Kulingana na mchungaji wa kanisa hilo Emmanuel Kipuno, Elizabeth Nalem aliondoka katika kanisa hilo na kujiunga na lingine baada ya uongozi wa kanisa hilo kupinga mienendo yake.
Kipuno amesema kanisa la Full gospel haliungi mkono tukio kama hilo wala kutoa mafundisho kama hayo kwa waumini wake bali lina taratibu zake kuambatana na imani pamoja na mafundisho kikristo.
Ikumbukwe wakati akijifanyia harusi mmewe mama huyo Joshua Nalem alidai mkewe alibadili mienendo yake kutokana na dhehebu analoshiriki akimhusisha na kanisa hilo la Full gospell