KANISA LA ACK KAPENGURIA LAPATA DAYOSISI MPYA HUKU MIZOZO YA MUDA IKITARAJIWA KUFIKA KIKOMO.

Huenda migogoro ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika kanisa la kianglikana dayosisi ya kaunti hii ya pokot magharibi ikafika mwisho.
Haya ni kulingana na seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi Samwel Poghisio baada ya ziara ya askofu mkuu wa kanisa hilo nchini Jackson ole sapit kaunti hii na kutangaza kubuniwa dayosisi ya pokot magharibi na kuwa ndiye atakayekuwa askofu wa dayosisi hiyo hadi litakapopata askofu mpya.
Poghisio ambaye ni mmoja wa Waumini wa kanisa hilo ametoa wito kwa waumini kushirikiana na kumaliza tofauti zilizopelekea kuibuka makundi mawili ili kupata mwelekeo wa uongozi wa dayosisi hii hasa baada ya askofu ole sapit kusema kuwa hilo litaafikiwa tu baada ya kupatikana mwafaka.