KAMUREN ATIA SAINI MKATABA NA WASOMI BARINGO KUSINI KATIKA JUHUDI ZA KUPIGA JEKI AZMA YAKE KUHIFADHI KITI CHA UBUNGE ENEO HILO.


Mbunge wa Baringo kusini kwenye kaunti ya Baringo Charles Kamuren ameahidi kwamba uongozi wake utazingatia utoaji wa huduma kwa wakazi iwapo atachaguliwa afisini kwa mara ya pili katika uchaguzi wa agosti 9.
Akiongea baada ya kutia saini mkataba wa maelewano na wasomi wa eneo bunge hilo chini ya muungano wa mogoswok kamuren amesema kuwa uongozi wake utahakikisha wakazi wanafaidi moja kwa moja.
Na kama njia ya kuhakikisha kwamba anafanikisha hilo kamuren ambaye analenga kutetea wadhifa wake kupitia chama cha UDA amesema kuwa atakua anaandaa mkutano kila mwaka ili kutathmini mafanikio ya uongozi wake.
Baadhi ya mapendekezo ya wasomi hao ni pamoja na kuzinduliwa kiwanda cha koriema alovera, kuwaunganishia wenyeji pamoja na taasisi kama vile shule umeme, kufufuliwa kwa chama cha ushirika cha wafugaji wa nyuki cha mogoswok miongoni mwa maswala mengine.