KAMPUNI YA NEW KCC YAAHIDI KUIMARISHA ZAIDI MKULIMA WA NG’OMBE WA MAZIWA.


Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya New KCC Nixon Sigey amesema shirika hilo la maziwa nchini kwa ushirikiano na wizara ya kilimo limeweka mikakati kuhakikisha kuwa mkulima wa maziwa anapata bei bora zaidi.
Akihutubu kwenye maonyesho ya kilimo eneo bunge la Cherangani Kaunti ya Trans-Nzoia Sigey amedokeza kuwa kwa sasa shirika hilo inaelekea kuchukua maziwa kutoka kwa wakulima kwa shilingi 45 kwa lita, akikariri ushirikiano wa serikali na mashirika ya binafsi katika kuandaa hafla za mafunzo kuhusu teknolojia mpya katika sekta ya kilimo nchini.
Aidha Sigey amesema uzalishaji wa maziwa kutoka kwa wakulima ungali chini, akiongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kusaidi kuinua uzalishaji huo, hii ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama ya bei ya
vyakula kwa mifugo mbali na kuondoa ushuru kwa bidhaa hizo.