KAMPUNI YA KENYA POWER KAUNTI YA POKOT IMEAHIDI KUREKEBISHA VIZINGITI VYA STIMA KAUNTI NZIMA

Kampuni ya umeme Kenya power kaunti hii ya Pokot magharibi inakabiliwa na changamoto kuhusu vizingiti vya stima ambavyo havidumu kwa kipindi kinachotarajiwa kufuatia athari za mchwa.
Kulingana na meneja wa kampuni hiyo kaunti hii Milimo Amusavi uwepo wa mchwa maeneo mengi ya kaunti hii umepelekea vizingiti hivyo kudumu kwa kipindi cha chini ya miaka miwili hali ambayo inaifanya kampuni hiyo kugharamika pakubwa kuweka vizingiti hivyo kila mara.
Wakati uo huo Amusavi amesema kuwa wana ufahamu kuhusu vizingiti ambavyo vinakaribia kuanguka maeneo mbali mbali ya kaunti hii akiwahakikishia wakazi wa maeneo hayo kuwa hali hiyo itashughulikiwa.
Aidha amesema mikakati inaendelea ya kutumia vizingiti vya saruji ili kukabili tatizo la mchwa.