KAMISHINA WA BUNGOMA AONYWA DHIDI YA KUINGIZA SIASA KATIKA VITA DHIDI YA DHULUMU ZA JINSIA.


Kamishina wa kaunti ya Bungoma Samwel Kimiti ameonywa dhidi ya kutumia afisi ya kupambana na dhuluma dhidi ya wasichana wadogo kuendeleza ajenda za kisiasa kwa baadhi ya wanasiasa kaunti hiyo.
Akizungumza na wanahabari katika afisi yake eneo la ndengelwa eneo bunge la Kanduyi, mwakilishi kina mama katika kaunti hiyo Catherine Wambilianga amesema kuwa Kimiti alipanga mkutano wa kuzindua kampeni ya kupambana na dhuluma za kijinsia na mimba za mapema katika afisi yake pamoja na mkewe gavana wa kaunti ya Bungoma Carolyne Wangamati bila kumhusisha.
Wambilianga amesema afisi yake imeweka mikakati ya kuhakikisha visa vya mimba za mapema pamoja na dhuluma za jinsia katika kaunti hiyo vinapungua huku akitaka maswala ya siasa kutoingizwa katika vita hivyo.