KAMATI ZA KUSIMAMIA MIRADI ZATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA BAADA YA KUSAMBAZWA FEDHA ZA CDF KACHELIBA.


Kamati ya hazina ya maendeleo ya maeneo bunge CDF eneo bunge la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi imesema kuwa imesambaza fedha zote kwa akaunti za kamati zinazosimamia miradi mbali mbali inayotekelezwa katika eneo hilo.
Akizungumza na kituo hiki meneja wa kamati hiyo Wilson Kurungura amesema kuwa kwa sasa jukumu ni kwa kamati mbali mbali ambazo zinasimamia miradi hiyo kuhakikisha kuwa zinatumika vyema na kuhakikisha inakamilishwa kwa wakati.
Korungura amesema kuwa kwa sasa kamati yake inatafakari kuhusu kuwasilisha maombi kwa wakati kwa serikali kuu ili kutuma fedha zingine kufanikisha miradi zaidi, huku akipongeza kamati ambazo tayari zimekamilisha baadhi ya miradi eneo bunge hilo.