KAMANDA ATAKIWA KUELEZEA ANACHOFAHAMU KUHUSU KUVURUGWA MIKUTANO YA RUTO.
Tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC pamoja na idara ya upelelezi DCI zimetakiwa kumwagiza mbunge maalum Maina Kamanda kurekodi taarifa kuelezea anachofahamu kuhusu madai aliyoibua kuwa naibu rais William Ruto ndiye anayevuruga mikutano yake kwa kutumia vijana.
Ni wito unaotolewa na wandani wa Ruto katika kaunti ya Trans nzoia wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Kinyoro Lawrence Mokosu ambao aidha wameshutumu vikali kuvurugwa mikutano ya kisiasa ya naibu rais maeneo mbali mbali ya nchi.
Wakati uo huo Mokosu amemtaka rais Uhuru Kenyatta kutoegemea upande wowote wa kisiasa na badala yake kuonyesha usawa wa wagombea wote huku akitoa wito kwa vijana kutokubali kutrumika visivyo na wanasiasa hasa wakati huu taifa linapokaribia uchaguzi mkuu.