KACHAPIN ATOA ONYO KALI DHIDI YA WAFANYIKAZI HEWA.


Gavana wa kaunti ya Pokot maghaibi Simon Kachapin amesema kuwa seikali yake itafanyia ukaguzi wafanyikazi wake.
Kachapin amesema kuwa ilivyo kwa sasa kaunti hii ina wafanyikazi wengi hewa ambao wanapokea mishahara kutoka kwa serikali hali hawatoi huduma yoyote kwa umma.
Aidha Kachapin amesema watu hao wamekuwa wakilipwa mishahara kutokana na uaminifu wao kwa wanasiasa fulani kaunti hii akionya kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya wale wanatakaopatikana wakihusika uovu huo.
“Pokot magharibi ni moja ya kaunti ambazo zinalipa kiwango kikubwa cha mishahara. Sasa nitafanya ukaguzi wa wafanyikazi kwa kuwa kuna taarifa kwamba tuna wafanyikazi hewa wengi katika serikali ya kaunti wanaolipwa mishahara ila hawatoi huduma zozote.” Alisema.
Wakati uo Kachapin amesema atahakikisha wote waliofuja mali ya umma wanakabiliwa kwa mujibu wa sheria, akisisitiza kwamba sekta zote za umma ambazo zimeghatuliwa sharti zitoe huduma bora kwa wananchi na kuboresha maisha yao.
“Yeyote atakayepatikana alitumia vibaya mali ya serikali sitasita kuchukua hatua kwa kuwa kuna sheria za nchi ambazo kila mfanyikazi wa umma anapasa kufuata. Ni lazima kila afisa wa serikali atumie vyema raslimali za serikali.” Alisema.